Home » » KAIKE PROMOTION IMENDAA PAMBANO LA NGUMI LA UBINGWA WA TAIFA

KAIKE PROMOTION IMENDAA PAMBANO LA NGUMI LA UBINGWA WA TAIFA

Written By peterdafi.blogspot.com on Friday, June 29, 2012 | 9:10 AM

Kaike promotion imeandaa pambano lingine la ubingwa wa taifa kati
BAINA MAZOLA na JUMA FUNDI(ambae alishawahi gombea mkanda wa dunia
nchini philipines) litakalopigwa jumapili ya tarehe 15 mwezi wa

saba,pambano hili ni mtiririko wa mapambano ya ubingwa wa ngumi na
kuendeleza vipaji vya mabondia chipukizi na wale tunaowategemea kwenda
kuchukua mikanda mikubwa ya dunia.

Inafahamika wazi kwa taifa letu,mchezo wa ngumi ni miongoni mwa mchezo
unaopeperusha vema bendera ya Tanzania lakini ni mchezo usio na
wafadhili wala wadhamini unajiendesha wenyewe kishidashida bila ya
utaalam mzuri wa uongozi utaalam upo katika uchezaji na mchezo
unaohitaji msaada wa hali ya juu sana kuinuliwa.wadhamini
wangejitokeza kudhamini ngumi wangelisaidia sana taifa letu.
mchezo wa tarehe 15july utasimamiwa na Tpbo na mapambano yamepangwa na
ibrahim kamwe chini ya uratibu wa kaike siraju yataongozwa na
mapambano ya utangulizi kati bondia anaechipukia kwa kasi issa
omar(toka bigright boxing mwananyamala) na Ramadhan kumbele bingwa wa
taifa toka kambi ya matumla-keko.
Anthony Mathias(aliyekuwa bingwa wa PABA) ataminyana na chipukizi
mwaite juma(toka bigright boxing)

mapambano mengine ni kama ifuatavyo hapo chini  na katika picha ni
issa omar akinolewa na mwalimu wake Ibrahim bigright

DATE; 15 / 07 / 2012
VENUE; DDC Kariakoo, Dar Es Salaam, TANZANIA
PROMOTER; Kaike Promotion
MATCHMAKER; Ibrahim kamwe
TICKETS; +255 715 707777

Bantam weight - Juma Fundi v/s Baina mazola - 10 round ,TPBO title
Fly weight- Ramadhan Kumbele v/s Issa Omar - 6 round
Bantam weight - Anthony Mathias v/s Mwaite Juma - 6 round
super feather weight - doi miyeyusho v/s shaban mtengela 6 round
light weight - Bakari mohamed v/s sadiki momba - 6 round
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger