Wanachama wa MRC
Watu 11 wanaoshukiwa kuwa
wanachama wa kundi haramu la Mombasa Republican Council (MRC) wameuwawa
katika eneo la msitu wa Bamba eneo la Kilifi katika Mkoa wa Pwani.
Mkuu wa Polisi eneo la Pwani ya Kenya Bwana
Aggry Adoli amethibitisha tukio hilo akisema kuwa wanakijiji waliwaona
watu walioshukiwa kuwa wanachama wa MRC wakiingia msituni na kuwafuata
na kisha kuwaua baadhi ya watu waliokuwa kwenye kundi hilo.Walikamatwa na silaha za kijadi kama vile panga na visu. Polisi wanasema kuwa mmoja wao alikuwa mganga wa kienyeji
Eneo la Pwani mwa Kenya limekuwa na migogoro ya kila aina kuanzia kwa uhasama kati ya jamii hasimu zinazoishi pembezoni mwa mkoa huo.
Polisi wamekua wakilaumiwa kwa kukosa kudhibiti ulinzi mkoani humo hasa wakati huu wa heka heka za maandalIzi ya uchaguzi utakaofanyika mwezi Machi mwaka ujao.
Hata hivyo bwana Adoli anasema kuwa utovu wa usalama sio kosa la polisi bali ni kutokana na matatizo yanayokumba jamii za eneo hilo.
Post a Comment