Helen Joseph, bondia mwanadada
ambaye anaishi katika jiji la Accra, nchini Ghana akipigana ngumi yuko mboni
kupanda kilele cha mafanikio katika maisha yake ya ngumi. Ni wakati ambao Helen
Joseph anayetoka katika nchi ya Nigeria aliokuwa anaungojea katika maisha yake
ya ngumi.
Helen Joseph akipozi kama bondia
Mwaka jana alikutana na bondia Dahianna
Santana katika jiji la San Domingo, nchini Dominican Republic kugombea ubingwa
wa dunia wa IBF katika uzito wa Unyonya (Fearherweight). Taabu na kashikashi zote
alizozipata wakati wa patashika ile ya mwaka jana zimekuwa fundisho tosha kwa
Helen wakati anapojiandaa kukutana na Marianna Gulyas kutoka nchini Hungary kugombea
ubingwa wa IBF wa mabara katika uzito wa unyoya.
Mpambano huo, unaoandaliwa na
kampuni maarufu ya kukuza ngumi ya GoldenMike Boxing Promotion Syndicate ya
nchini Ghana unategemea kuwa wa patashika kweli kutokana na mabondia wote
wawili kuwa na ujuzi tele ulingoni. Wawili hawa watakutana tareeh 30 March
katika uwanja wa michezo wa Accra na mpambanohuu utarushwa moja kwa moja na luninga
ya Super Sports.
Ni mapromota wachache na mameneja
wachache ambao wanaweza kuwekeza kiasi
kikubwa hivyo cha pesa katika mchezo wa ngumi namna ambapo kampuni ya
GoldenMike Boxing Promotions Syndicate ya nchini Ghana imewekeza katika kuinua
kipaji cha mwana dada Helen Joseph.
Kwa upande wake Helen ambaye ni
nadhifu, mtanashati na mwenye nidhamu ya hali ya juu, mchezo wa ngumi ndio
unaomlisha katika maisha yake na atatumia uwezo wake wote kuhakikisha kuwa taji
hli kubwa la ngumi linabaki barani Afrika na kulitumia kama ngazi ya kukutana
tena na Dahianna Santana katika ubingwa wa dunia!
Post a Comment