Tangu Rais JAKAYA KIKWETE aanze kuwa rais wa nchi hii amepitia kipindi kigumu sana cha uongozi kutokana na chokochoko toka kwa makundi mablimbali ambayo mengi yalijificha kwenye migongo ya makundi mengine kwa kuwa hayakuwa na mamlaka kumtuhumu waziwazi Rais wa nchi. Makungi kama Jukwaa la Katiba, Mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP), kituo cha Sheria na haki za binadamu(LHRC), Chama cha wanawake wanasheria Tanzania(TAWLA) na NGO nyingine kama hizo kwa mujibu ya malengo ya kuwanzishwa kwazo hazikuwa na mamlaka yoyote kisheria kupiga propaganda kumsakama Raiswa nchi kwa vile Rais anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya nchi na yote aliyoyafanya amefanya hivyo kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Jambo la ajabu ni kwamba taasisi hizo zilitumia taasisi zingine na hasa vyama vya siasa kumshambulia Rais kwa hoja ambazo hazikuwa na nguvu, mbaya kabisa ni pale wanasiasa walidiriki hata kutumia maneno ambayo kwa mujibu wa kATIBA yetu walivunja sheria ya kumtukana Rais wa nchi. Lawama kama "RAIS AMESHINDWA KUWASHUGHULIKIA WAHALIFU" , Maneno kama "RAIS NI DHAIFU" "NCHI HAITATAWALIKA", zote hizi zimekuwa ni hoja ambazo hazina nguvu na uvunjifu wa sheria kwa vile sote tunatambua kuwa nchi yetu inaongozwa kwa kufuata utawala wa sheria.

Lakini Watanzania wengi wamekuwa wkijiuliza ni nini hasa kinachopelekea baadhi ya vyama vya siasa, Taasisi zisizo za kiserikali , makundi fulani fulani nchni kuwa na tabia hii ya kutoheshimu Serikali na kuizushia mambo, kuchochea vurugu na hata kutoa matamshi yenye kuhatarisha amani ya nchi yetu.

Mchakato wa Katiba Mpya umekuja kuwafungua macho watanzania kuwa kumbe, hizi taasisi ambazo zimekuwa zikiwatumia viongozi wa vyama vya siasa kuwapotosha watanzania, kuchochea vurugu na hata kuwa na ujasiri wa kutoa matamko ambayo yanaweza kuhatarisha amani zote kwa pamoja, zinapata pesa kutoka maeneo yanayofanana ndani na nje ya nchi.

Itakumbukwa kuwa, hivi majuzi Wabunge wa Upinzani waliingizwa mkenge na chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo (CHADEMA) kususia mswada wa sheria ya Marekebisho ya bunge la Katiba, hoja zao za msingi zikiwa ni mbili ambazo ni kutokubaliana Rais kuteua wajumbe 166 wa bunge la Katiba na Wazanzibari kutoshirikishwa katika maoni ya RASIMU ya Katiba mpya, hoja ambazo hata hivyo zilionekana ni za uongo baada mawaziri wanaohusika na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya sheria kujibu madai hayo.

Binafsi nilitegemea hoja ya wazanzibari hawakuhusishwa kwenye kutoa maoni ingepewa uzito kwa vitendo kwa kuanzia mikutano yao Zanzibar na ziyo bara.

Mpango huu wa CHADEMA kuwashawishi wapinzani waungane katika kususia mswada huu, unaibua hisia ni jinsi gani NGOs kama TAWLA, GDSS, LHRC, TGNP na nyinginezo zilivyokuwa zinajificha kwenye mgongo wa CHADEMA kuhakikisha mchakato mzima wa kupatikana kwa Katiba mpya unavurugika.

Matukio haya yanadhihirisha wazi kuwa kuna makundi yalijipanga na kuna makundi yameingizwa mkenge kwenye muungano wa huu ambao sasa tunashindwa tuupe jina gani, muungano wa Wapinzani au muungano wa CHADEMA, CUF, NCCR, TGNP, LHRC, GDSS, TAWLA ambapo leo wamekutana viwanja vya Ofizi za TGNP, Mabibo:

1. Alianza TINDU LISSU kukiita chama cha CUF kuwa ni cha Wazanzibari;
2. CHADEMA wakaja na hoja kuwa ZANZIBAR hawakushirikishwa na wakaanza kutoka nje ya ukumbi huku wakiangalia pembeni kuona kama CUF wanawafuata, na walipoona wameingia mkenge wakapiga makofi na kusema wajinga ndiyo waliwao;
3. Siku moja baada ya kutoka nje ya ukumbi wa bunge, Gazeti za MAWIO likaja na kichwa cha habari kinasema "CHADEMA, CUF na NCCR wakutana , kuishitaki Serikali kwa Wananchi" wakati ni kila chama kilikutana peke yake;
4. Siku iliyofuata ndipo Viongozi hao walikutana kuhalalaisha taarifa ya MAWIO;
5. Jana Tarehe 17/09/2013 muungano huu wa wapinzani wakiongozwa na viongozi wengi wa CHADEMA wakakutana ofisi za Jukwaa la Katiba huku vyma vya CUF na NCCR vikiongozwa na wenyeviti pekee.
6. Leo Tarehe 18/2013 wakekutana ofisi za TGNP

Ukiangalia mtiririko huo wa matukio hauoni jinsi gani ZANZIBAR inahusishwa.


MIMI NASEMA, JAKAYA KIKWETE ni lazima asaini mswada huu ili Watanzania tujue kilichojificha nyuma ya Pazia. Tujue kama kuna watu toka nje wanataka kulitumbukiza taifa kwenye machafuko kwa kisingizio cha Katiba mpya, Kinga ni bora kuliko Tiba, JK katika Katiba Mpya, "ULIAMUA, UKATHUBUTU sasa MALIZIA" watanzania wengi tuko nyuma yako.