Home » » NDEGE YAANGUKA MBUGANI SERENGETI NA KUUWA WATU WATATU.

NDEGE YAANGUKA MBUGANI SERENGETI NA KUUWA WATU WATATU.

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, September 2, 2014 | 2:20 AM

NDEGE YA KENYA YAANGUKA TANZANIA,YAUA WATU WATATU

Ndege ya Kampuni ya Safari Express Limited imeanguka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuwateketeza watu watatu waliokuwamo ndani.

Ndege hiyo yenye namba za usajili 5Y-SXP iliruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza Jumapili saa 1:26 usiku ikielekea Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) Kenya ambako ilitakiwa kutua saa 2:36 usiku.

Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Paschal Shelutete alikiri ndege hiyo kuanguka kwenye hifadhi hiyo na walikuwa katika harakati za kuitafuta.

Mkaguzi Mkuu wa Ajali za Ndege nchini, kutoka Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, David Nyamwihura alisema ajali hiyo ilitokea takriban maili 20 kutoka Serengeti, katika eneo la Kogatembe na watu wote watatu waliokuwamo wamefariki dunia.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger