Home » , » Picha, MASHABIKI WALIVYOFANYA FUJO KTK SHOW YA DIAMOND PLATINUM, UJERUMANI.

Picha, MASHABIKI WALIVYOFANYA FUJO KTK SHOW YA DIAMOND PLATINUM, UJERUMANI.

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, September 2, 2014 | 2:26 AM

MASHABIKI WALIVYOFANYA FUJO KWENYE SHOO YA DIAMOND,UJERUMANI

Usiku wa Jumamosi ya Tarehe 30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri.Mwanamuziki nyota wa Bongo Flava Nasib Abdul 'Diamond Platnumz' alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani, baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.

Washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake Mr.Awin Williams Akipomiemie raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.

Hapo ndipo washabiki hao walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake.

Kilichowakera zaidi mashabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kuvunja vyombo vya muziki ma-Djs walishambuliwa na wapo hosptalini kwa sasa.

Moja wa Djs hao alipoteza Lap top yake, mwanadada DJ Flor alipatwa mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospatal.

Polisi nchini Ujerumani wamesema tukio hilo la aibu halijawahi kutokea, kwani msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari sana kwani mashabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger