Vijana wa Chama cha Mapinduzi Leo hii Wameingia Siku ya Pili ya Matembezi ya Mapinduzi ya Zanzibar, Matembezi haya Ya Kusheherekea Miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalifunguliwa Jana na Naibu Kamanda Wa UVCCM Zanzibar na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM (MCC) na Makamo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh Barozi Seif Khalid.
Pia Alikuwepo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Mh Sadifa
Katibu Mkuu Wa UVCCM Taifa
Sekretelieti Nzima ya UVCCM Taifa
Wajumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa
Viongozi mbali mbali wa Chama Na Serikali.
Pia Makada Na WanaCCM wapenda Amani.
Uzinduzi huu wa Matembezi ulifunguliwa Nje ya Mji wa Zanzibar Kijiji cha Unguja Ukuu, Jimbo la Koani, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Juzi walitembea Kutoka Skuli ya Unguja Ukuu hadi Unguja Kuu Njia Nne, Na jana Waliendelea Kutoka Njia NNE hadi Skuli ya Uzini, Kijiji cha Uzini, Jimbo la Uzini, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini.
Hapo Vijana Walifanya Mapumziko hadi leo Terehe 08/01/2015 wataelekea hadi Kijiji cha Mahonda, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa Wa Kaskazini Unguja.
Matembezi yanaendelea mpaka Tarehe 10 Mwezi wa Kwanza 2015 Siku ya Kilele cha Matembezi haya, ambayo yanatarajiwa Kupokelewa Na Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Na Rais wa Zanzibar Na Mwenyekiti wa Baraza LA Mapinduzi Dr Ally Mohamed Shein, Katika Viwanja vya Maisara Jimbo la Kikwajuni, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Kichama.
Na Tarehe 12 Mwezi wa Kwanza 2015 Itakuwa ni Kilele cha Sherehe Hizo Kitaifa ambazo zinatarajiwa kufanyika ktk Viwanja vya Amani, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini.
Katika Sherehe Hizi Kutagubikwa Na Shughuli Mbali mbali za Burudani, Gwaride, Ngoma Mbali mbali pamoja na Maandamano ya Mikoa Mitano ya Zanzibar, Taasisi za Umma na Asasi za Kiraia Pamoja Na Hotuba ya Sherehe Hizo Kutoka Kwa Rais wa Zanzibar Na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
SHIME WATANZANIA TUJITOKEZENI KWA WINGI KATIKA SHEREHE HIZI, KUONYESHA UZALENDO WA TAIFA LETU.
KWANI KILA TAIFA LINAHISTORIA YA UPATIKANAJI WA UHURU WAKE, UHURU WA TAIFA LETU ULIPATIKANA TEHERE 12/01/1964 NA SIO 1963 KAMA WAPINGA MAPINDUZI WANAVYOELEZA KWA ZANZIBAR NA KWA TANGANYIKA ILIKUWA Ni TAREHE 09/12/1964
KWA UMOJA WETU, USHINDI LAZIMA, KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
MAPINDUZIIIIIII..........!!!!??
....DAIMAAAA....!!!!!!!!!!
1. TUTAYALINDA
2. TUTAYATETEA
3. TUTAYAPIGANIA KWA MASLAHI YA TAIFA, Potelea mbaliiiiii........!!
MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU YABARIKI MAPINDUZI YA ZANZIBAR.
Post a Comment