WAZIRI WA AFYA AMEWATAKA WANANCHI KUTAMBUA KIPINDUPINDU BADO KIPO NA WAJILINDE.
Dodoma.
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia Wezee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu ametembelea mnada (mnadani/Mnada wa Nyama Choma) eneo la Msalato Dodoma.
Waziri ametembelea Mnada huo kufuatilia ugonjwa wa kipindupindu unaendelea kusumbua katika baadhi ya Maeneo nchini Tanzania, na Moja kati ya maeneo hatarishi ni maeneo ya mikusanyiko ya watu na wanafanyiko kama minadani Nk...
Waziri wa Afya Amewataka wananchi kutambua kuwa kipindupindu bado kipo na kimesambaa sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Mkoani Dodoma. Hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha kipindupindu kinakwisha.
Ameyasema hayo akiwa anatambua kuwa ili kipindupindu kiishe kinahitaji kila Mtanzania ajue wajibu wake kuhakikisha kuwa tunalinda mazingira nakuwa wasafi kwa kila jambo ili kuwa Safi na salama. Aidha Waziri Ummy ameagiza kuendelea kwa Katazo la Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Dkt Jasmine Tiisekwa la Kuuza Nyama Choma Msalato hadi pale Uongozi wa Wilaya utakapojiridhisha kuwa ugonjwa wa kipindupindu umetoweka mkoani humo.
Pia ameutaka Uongozi wa Manispaa Dodoma kukaa na wafanyabiashara hao ili kuona ni jinsi gani wanaweza kuendelea na biashara zao huku wakizingatia Kanuni za Usafi wa Afya na Mazingira.
Toka kuteuliwa kwake Waziri Ummy amekuwa mfuatiliaji wa mambo kwa kina na kwa umakini mkubwa tangu ateuliwe. amefanya ziara nyingi za kustukiza na zile zakufuatilia Majukumu na Mienendo ya utendaji katika wizara yake.
Huu umekuwa mwanzo mzuri wa serikali hii ya Awamu ya Tano katika kutimizwa kwa kauli mbiu ya Mh Rais ya HAPA KAZI TU.
Post a Comment