Home » » Waziri Jaffo Asema Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Inanuka Ufisadi.

Waziri Jaffo Asema Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Inanuka Ufisadi.

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, March 16, 2016 | 9:16 AM

Waziri Jaffo: Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Inanuka Ufisadi

Naibu Waziri wa Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jafo amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya inanuka ufisadi unaofanywa na baadhi ya wakuu wa idara.

Kauli hiyo ya waziri inatokana na tuhuma za upotevu wa zaidi ya Sh800 milioni mwaka 2010/2011 zilizolenga kuboresha elimu ya sekondari wilayani Mbarali.

Fedha hizo ambazo zinaweza kutengeneza madawati 1,600 yanayotosheleza mahitaji ya wanafunzi 4,800, ikiwa dawati moja kwa bei ya soko kwa sasa ni Sh50,000 zilifujwa na watumishi ambao miongoni mwao bado wapo.

Jafo alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza na wakuu wa idara, watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo kwenye ziara yake iliyolenga kutoa maelekezo ya kiutendaji.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Yeremiah Mahinya alimhakikishia Jaffo kwamba watatekeleza maagizo waliyopewa kwa ufanisi na kwa muda, ikiwamo kuondokana na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Mkuu wa wilaya hiyo, Gullamhusein Kiffu alisema mtumishi atakayeshindwa kutimiza majukumu vizuri atamchukulia hatua.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger