Home » , » DC HAPI ATEMBELEA GHAFLA HOSPITALI YA MWANANYAMALA USIKU LEO

DC HAPI ATEMBELEA GHAFLA HOSPITALI YA MWANANYAMALA USIKU LEO

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, May 4, 2016 | 2:52 PM

DC HAPI ATEMBELEA GHAFLA HOSPITALI YA MWANANYAMALA USIKU LEO
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Salum Hapi leo usiku ametembelea hospitali ya Mwananyamala kujionea utoaji wa huduma hasa wakati wa usiku.

Hapi ambaye alitinga hospitali hapo kama mgonjwa wa kawaida akivalia kofia ya mkeka alitembelea mapokezi, vyumba vya daktari na baadae kumshtukiza kiongozi wa madaktari kwa usiku huo ofisini kwake akimuelekeza kumtembeza sehemu mbalimbali za hospitali hiyo ambayo Mkuu wa wilaya alitaka kuziona.
Mh. Hapi alitembelea wodi ya watoto, wanaume, wodi ya kina mama, wodi ya dharura (emergency) na kumalizia chumba cha kuhifadhia maiti (mortuary) ambako alizungumza na wagonjwa, kuwajulia hali na kujionea changamoto zinazowakabili.
Akiwa chumba cha kuhifadhia maiti Mh. Hapi alifanya mazungumzo na mhifadhi maiti na kujua changamoto zinazoikabili ofisi yake.
Hospitali ya Mwananyamala inatajwa kuwa na changamoto nyingi za utoaji huduma hali inayosababisha malalamiko ya mara kwa mara ya wananchi.

Hapa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aliingia nakujipanga ktk Dawati la wagonjwa wanaongoja kuingia Kwa Dr kusikilizwa!

Hatimae Wagonjwa walipungua na akabakia mama Mmoja ambae baada ya mama kuingia DC Hapi alifuata kuingia kwa Dr wa Zamu alokuwapo OPD.

Baada yakuzungunza na Dr Alimuelekeza nakujitambulisha Kuwa yeye ni Mkuu wa Wilaya na angependa kujua hali ya Huduma na wagonjwa ikoje!
Ivo aliomba kutembelea Wodi za wagonjwa kisha Msafara ukaanza kutembelea Wodi hizo.
DC alifika Wodi ya Wanaume nakujionea Changamoto za ukosefu wa Neti, Mashuka na Upungufu wa Vitanda kwa Baadhi ya Wodi.
DC Hapi alipotoka alikwenda Nje ya Hospitali nakununua Dawa, Kisha Kudai Risiti Jambo ambalo Lilizua Mtafaruku kwa Mama Muuza Duka, Mama alitoa maneno makali na yakejeli kwa Kumwambia DC Kuwa hana Risiti kama Hataki Alete Dawa amrudishie Pesa yake.
Ndipo DC alipobadilika nakumkalipia Mama Kabla hajajua Nani anazungumza nae akastuka na kutoa Risiti.


Pozi la DC Hapi akingoja Mama anaandika Risiti
Mama Muiza Duka la Dawa akiandika Risiti
Picha Hii inaonyeaha DC Hapi akiwa amesimama na Dr  aliekuwa akimtembeza na hapa ni Mlango wakuingia Mochwali Alikuta Magodolo yako pale na kuna Wagonjwa wanalala Chini ivo akahoji Vipi Magodolo yako pale na kuna watu wanahitaji.
Jibu likawa Yale yako matengenezoni kwa kuyawekea Makava.
DC Hapi akizungumza na Bwana Ally Mbwambo muudumu wa Chumba chakuhifadhia Maiti.
Alijielezea nakusema Chamoto ktk Kitengo chake kwa sasa ni Kuwa Jokofu moja limeharibika ivo wanatumia Dawa sana Kuhifandi Miili.
Lakini pia Chumba huwa kidogo kama Inatokea Ajali kwa wingi na Panapotokea Police Kesi ambazo Miili inakuwa haitike haraka ivo huihamisha nakupeleka Muimbili nk..
DC alimaliza Ziara yake yakustukiza kwa Kuwa kugundua Mapungifu ya NET, MASHUKA NA UPUNGIFU WA MADAKTARI, kwani Usiku hu Wahudumu kila Mahala ni mmoja mmoja itakuwajw kama Emergence itatokea.
Ivo DC amenote na anakwenda kushulkia kero na changamoto hizo.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger