Home » » RAIS MAGUFULI AWASIFU RC MAKONDA NA DC HAPI KWA UCHAPAKAZI

RAIS MAGUFULI AWASIFU RC MAKONDA NA DC HAPI KWA UCHAPAKAZI

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, June 2, 2016 | 10:34 AM

RAIS MAGUFULI AWASIFU RC MAKONDA NA DC HAPI KWA UCHAPAKAZI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli leo akiwa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam amewasifu na kuwaelezea Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi kuwa ni vijana wachapakazi na makini katika kuhakikisha mambo yanakwenda.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo akizungumza na maelfu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na wanajumuiya wa chuo hicho kuhusu masuala mbalimbali ya elimu nchini. Akizungumzia matunda ya elimu ya juu na hasa chuo Kikuu cha Dar es salaam katika kupika viongozi,  Rais Magufuli aliwataja Mh. Hapi na Makonda kama mfano wa vijana hodari na wachapakazi.
"Nimemuona Kaimu Mkuu wa Mkoa Mh. Hapi na Makonda, hawa ni vijana safi na wanafanya vizuri sana. Wanaforce mambo na wanahakikisha yanakwenda."

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda hakuweza kuhudhuria kutokana na kuwa na majukumu mengine.
Rais Magufuli ameahidi kutoa Shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kuwaasa wasome kwa bidii na kukataa kutumiwa na wanasiasa.
Raisi Dr. Magufuli anakua Rais wa kwanza kuzungumza na hadhara kubwa ya wanafunzi wa Chuo Kikuu tangu kuanzishwa kwa chuo hicho miaka 55 iliyopita. Wanafunzi na wanajumuiya zaidi ya 6000 walikusanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu kusikiliza hotuba ya Rais Magufuli.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger