Marekani imesema kuwa iko tayari kuchunguza shambulizi la bomu lililomuua mkuu wa ujasusi nchini Lebanon.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, waziri wa
mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton pamoja na waziri mkuu wa
Lebanon Najib Mikati wamekubaliana kuhusu uchunguzi wa pamojaMakabiliano yalizuka baada ya mazishi ya afisaa huyo siku ya Jumapili, huku waaandamanaji wakimtaka bwana Mikati kujiuzulu.
Mjini Beirut, Polisi waliwafyatulia risasi na gesi ya kutoa machozi waandamanaji hao walipokuwa wakijaribu kuvamia ofisi za serikali mjini humo.
Kuna ripoti kuwa huenda ghasia zaidi zikatokea Kusini na Magharibi mwa Beirut.
Viongozi wa upinzani wamelaumu nchi jirani ya Syria kwa mashambulizi hayo.
Idadi kubwa ya maafisa katika serikali ya Lebanon wanaunga mkono serikali ya Syria.
Aidha serikali ya Syria imelaani shambulizi hilo ambalo pia liliwaua walinzi wa bwana Hassan pamoja na mwanamke mmoja aliyekuwa karibu na eneo la shambulizi.
Mnamo siku ya Jumapili, Bi Clinton alisisitiza kujitolea kwa Marekani kuhakikisha uthabiti wa Lebanon, uhuru wake na muhimu kabisa usalama
Clinton ,aligusia umuhimu wa viongozi wa kisiasa kushirikiana wakati huu ili kuhakikisha hali ya utulivu inaimarishwa na kwamba wale waliohusika watawajibishwa kwa kuchukuliwa hatua za kisheria. .
Post a Comment