Polisi nchini Kenya wamekabiliana na waandamanaji waliozingira
majengo ya bunge kulaani jaribio la wabunge kutaka kujiongeza mishahara.
Polisi hao wametumia gesi ya kutoa machozi pamoja na maji kuwatawanya
waandamanaji hao ambao wengi wao ni wanachama wa mashirika ya kijamii ambao
wamesma katu hawaondoki katika majengo hayo ya bunge hadi wabunge watakapopata
ujumbe wao.Mashirika ya kijamii yaliandaa maandamano hayo kuonyesha ghadhabu waliyonayo wakenya dhidi ya wabunge hao wanaotaka kuongezwa miashara, miezi miwili tu baada ya kufanyiika uchaguzi mkuu wa amani.
Aidha waandamanaji hao walipeleka Nguruwe kwenye mlango mkuu wa kuingia katika bunge pamoja na damu kama ishara kuwa wabunge ni watu walafi na wasiojali maslahi ya wakenya kwa kujitakia makubwa.
Maandamano haya yanakuja siku moja baada ya tume ya kitaifa ya mishahara ambayo wajibu wake ni kudhibiti mishahara ya wafanyakazi wa umma kusema kuwa katu haitawaongeza mishahara wabunge.
Tume hiyo ilisema siku ya Jumatatu kuwa haitaogopa vitisho vya wabunge kutaka kuivunjilia mbali tume hiyo ikiwa hawatawaongeza mishahara wabunge kama kikwazo.
Wabunge hao walijaribu kwa kutumia vitisho kuilazimisha tume hiyo kuwoangeza mishahara lakini hawakufua dafu.
Ni baada ya mbunge mmoja kuwasilisha hoja bungeni kuwa ikiwa tume hiyo haitawaongeza mishahara watafanyya kila hali kuivunja.
Hata hivyo tume hiyo ni ya kikatiba.
Wabunge wa Kenya wanataka kulipwa mshahara wa shilingi 850,000 wakati wakihudumu katika bunge la kumi ikipuuza mshahara waliowekewa na tume ya mishahara ambao ni shilingi 532,000. Wanasema pesa hizi ni kidogo sana.
Post a Comment