Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mathias Chikawe, (katikati) Mwakilishi
wa Balozi wa Saud Arabia, pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP
Ernest Mangu, wakitiliana sahihi moja kati ya Hati za makabidhiano ya
magari 20 aina ya Toyota Land Cruiser pamoja na pikipiki
40 vilivyotolewa na serikali ya Saud Arabia, vitendeakazi ambavyo
vitasaidia katika kuongeza kasi na ufanisi katika kupambana na matukio
ya uhalifu na wahalifu.(picha na Demetrius Njimbwi wa Jeshi la Polisi ).
Baadhi
ya magari aina ya Toyota Land Cruiser yaliyotolewa na serikali ya Saud
Arabia na kukabidhiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kupitia Jeshi la
Polisi Nchini, magari hayo 20 pamoja na pikipiki 40 zenye thamani ya
zaidi ya Dola Milioni moja huku magari hayo pamoja na pikipiki
zikitarajiwa kupelekwa katika baadhi ya vituo vya Polisi hapa nchini
ambavyo vinaupungufu wa vitendea kazi vya aina hiyo na kusaidia katika
kukabiliana na matukio ya uhalifu na wahalifu.
Baadhi
ya aina ya Pikipiki zilizotolewa na serikali ya Saud Arabia na
kukabidhiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kupitia Jeshi la Polisi
Nchini, magari hayo 20 pamoja na pikipiki 40 zenye thamani ya zaidi ya
Dola Milioni moja huku magari hayo pamoja na pikipiki zikitarajiwa
kupelekwa katika baadhi ya vituo vya Polisi hapa nchini ambavyo
vinaupungufu wa vitendea kazi vya aina hiyo na kusaidia katika
kukabiliana na matukio ya uhalifu na wahalifu.(picha nap Demetrius)
Post a Comment