Home » » Apigwa Risasi Maisha Club na Kupoteza Maisha

Apigwa Risasi Maisha Club na Kupoteza Maisha

Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, December 29, 2014 | 12:49 AM

Kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, leo
usiku amepigwa risasi ya shingo na watu wasiojulikana wakati akiingia
Club Maisha ilioko Oyster Bay jijini Dar es salaam.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa tano(5) usiku ambapo kijana huyu akiwa
na rafiki zake wanne(4) wakiwa ndio wanashuka kwenye gari yao waliokuja
nayo, walijikuta wamevamiwa na watu wawili wasiojulikana na yeye
kupigwa risasi ya shingo kisha watu hao kutokomea kusikojulikana.
Shuhuda wa tukio hilo alisema aliwaona watu wawili walioshuka kwenye
gari ndogo nyeusi ilifunga breki kwa kasi kwani walionekana walikuwa
mwendo kasi sana, kisha kuwavamia watu waliokuwa wanashuka kwenye
gari ilikuwa imepaki muda mfupi baada ya kufika eneo hilo. shuhuda huyo
aliendelea kwa kusema alisikia sauti ndogo ya kitu kilicholia "pyuuu!!!"
bila ya kuelewa ni nini na kisha kufuatiwa na kelele nyingi za watu hao
waliokuwa wamevamiwa. Waliotenda tukio hilo walitoweka mara moja eneo
la tukio baada ya watu kujaa eneo ambalo kijana huyo alipigwa risasi
alikuwa ameanguka chini.
Polisi walifika eneo la tukio na kukuta kijana huyo ameanguka chini na
damu nyingi zikiwa zimemtoka sehemu za shingoni na kifuani huku akiwa
amewekewa nguo shingoni ili damu isiendelee kutoka ambapo ilisemekana
ilikuwa ikitoka nyingi sana, walimpakia kwenye gari yao kumuwahisha
katika hospitali ya jirani ya mwananyamala, lakini kijana huyo alifia njiani
akikimbizwa kuelekea hospitali
Tukio hili linaonekana nila kulipiza kisasi ingawa taarifa kamili bado
hazijajulina, endelea kufatilia blog yetu kujua mwendelezo wa tukio hili la
kusikitisha.
185k

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger