Home » » Mh Mwigulu Nchemba aagiza Afisa Ardhi wa Wilaya ya Butiama Ndg Clavery Bitabile Akamatwe Mara Moja

Mh Mwigulu Nchemba aagiza Afisa Ardhi wa Wilaya ya Butiama Ndg Clavery Bitabile Akamatwe Mara Moja

Written By peterdafi.blogspot.com on Saturday, April 16, 2016 | 4:47 AM

BREAKING NEWS:

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba aagiza afisa ardhi wa wilaya ya Butiama ndg.Clavery Bitabile akamatwe mara moja na vyombo vya dola vichukue hatua kwa kosa la kuuza eneo la mnada wa upili(Mnada wa Mifugo) wa Kirumi uliopp wilaya ya Butiama.

Mbali na kuuza eneo hilo na kutoa hati kwa mtu binafsi wakati tayari eneo hilo la serikali la mnada lilikuwa na hati,Bwana Bitabile amekuwa kinara wa kusababisha migogoro kadha wa kadha katika wilaya ya Butiama na jimbo la msoma vijijini kwa muda mrefu Moja ya migogoro mikubwa anayotajwa kusababisha ni ule wa shamba la Buhemba(Mikamariro) n.k
Mwigulu Nchemba akitoa agizo hilo,amesisitiza pia vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa haraka ili mnada huo uanze kufanya kazi.

Hatua hii ni mwendelezo wa ziara ya Mh.Mwigulu nchemba kukagua maeno mbalimbali yanayohusiana na wizara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa.Jioni ya leo,mwigulu atakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara Tarime mjini kuzungumza na wananchi kuhusu dira ya wizara yake katika kuimarisha mfumo wa upatikanaji wa pembejeo,ufugaji wa kisasa na uvuvi salama.

(Picha Mwigulu nchemba akiwa eneo la tukio la mnada wa Upili-Kirumi Butiama.)

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger