Home » » Waziri Ummy Mwalimu Ampa Siku Tisini Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kahama Awe Amenunua XRay

Waziri Ummy Mwalimu Ampa Siku Tisini Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kahama Awe Amenunua XRay

Written By peterdafi.blogspot.com on Saturday, April 16, 2016 | 12:48 AM

Na.Catherine Sungura,

Kahama

Mkurugenzi wa halmashauri  wa mji kahama  amepewa siku tisini awe  amenunua mashine ya mionzi (x ray)kwa ajili ya hospitali ya mji kahama
Agizo hilo amepewa jana na Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy mwalimu wakati alipotembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa kada ya afya wa wmji huo.
Waziri Ummy alisema ametoa agizo hili ili kuweza  kurahisisha usumbufu wanaupata wananchi wa wilaya hiyo kwa kwenda kupata huduma  nje ya hospitali ambapo wakati mwingine vipimo hivyo vinakuwa havisomeki vizuri kwa kukosa viwango vinavyostahili za mashine hizo.
Hata hivyo waziri ummy alisema upatikanaji wa mashine hizo itapunguza malalamiko mengi toka kwa wananchi kwa ukosefu wa kifaa tiba hicho ili  kwani hospitali hiyo hivi sasa inahudumia wananchi zaidi ya milioni moja hususan toka wilaya zote za wilaya hii
Aidha, alizitaka halmashauri zote mjini kuweza   kuwekeza kwenye huduma za vifaa tiba  ambavyo inarahisisha kugundua  matatizo yanayowakabili wananchi wanaofika kwenye kupata huduma na hivyo kuwapatia matibabu stahili wagonjwa wanaofika kupata matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma nchini.
“siku hizi lazima muwekeze  kwenye kununua vifaa tiba ili kuweza kupata kutoa huduma nzuri ,pesa mnakusanya na kahama ni halmashauri tajiri,mkurugenzi  nakupa siku tisini uwe umenunua mashine hiyo
Naye mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Vita kawawa amemuahidi waziri huyo kwamba amepokea maagizo yote aliyoyatoa na atayafuatilia ili kuweza kutatua malalamiko ya wananchi na yale ya watumishi wa kada ya afya

Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto akiongea na baadhi ya wakazi wa kahama waliofika hospitalini hapo kuangalia wagonjwa wao

Mfamasia mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa shinyanga Luciano Lodrick akimpatia maelezo waziri wake me afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto jinsi ya utengenezaji wa maji tiba

Waziri.Ummy Mwalimu akitoa galvanize kwa wagonjwa waliofika kupata matibabu kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa.shinyanga

Waziri Ummy Mwalimu akiangalia kifaa cha kutengenezea maji tiba kwenye.hospitali ya.rufaa ya mkoa wa shinyanga

Mh.Ummy Mwalimu akiangalia matangazo yaliyobandikw kwenye ubao hospitanini hapo.Waziri Ummy ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kubandika gharama za matibabu pamoja na namba za simu kwa ajili ya kupokelea maoni na malalamiko toka kwa wananchi


Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh.Vita Kawawa(Katikati) akionesha kwa vitendo bango hilo linapotakiwa kuwekwa,kushoto ni Mh.Ummy Mwalimu na kulia ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji kahama Anderson Msumba
Mh.Ummy Mwalimu akiwaelekeza kamati ya afya ya wilaya ya kahama mahali linapotakiwa kuwekwa bango linaonesha huduma za wazee inapopatikana

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger