j
Dk. Hamisi Kigwangalla
ALIANZA KWAKUSEMA HIVI....!!!!
"Kuna watu wanaogopa sana kuwaza vitu vitu vikubwa, mimi si mmoja wao. Hata kufika tu hapa kwenye udaktari haikuwa rahisi (jambo lenye kuwezekana) lakini mimi niliamini inawezekana na nikapigana mpaka nikafika - na kwa hakika halikuwa jambo la ghafla, ama la kufikirika tu, lilikuwa ni jambo lililohitaji discipline, bidii na umakini wa hali ya juu - qualities ambazo nilikuwa nazo na hivyo sikupata t...
abu sana kufikia ndoto ile...leo ni daktari! Rafiki yangu George McKenzie na mke wangu (toka akiwa Girlfriend wangu) anafahamu, kuwa niliwaza sana kuwa Mbunge siku moja na ndoto hii ni ya siku nyingi, na ndiyo maana ilipokamilika nikaamua kufanya kazi kwa bidii kwelikweli, haikuwa rahisi kuwa Mbunge, ilihitaji uwe na pesa nyingi, uwe maarufu, uwe na nguvu na uvumilivu wa kutosha ili uweze kuwa Mbunge (mtu yeyote mwepesi wa kukata tamaa angeweza kuacha kabisa kuota kuwa MB) - sifa hizo nilikuwa nazo na sasa nimekuwa Mbunge! Leo hii nimeona watu wengi tu wa ajabu ajabu wanatamani kuwa 'Rais' wa nchi, nikaogopa na kushangaa sana, kwamba hata hawa wanatamani kuwa 'Rais' mbona ni wa ajabu ajabu sana, mbona hawafai kabisa - nikaona kama mimi ninawaona hao hawatoshi kuwa 'Rais' wa nchi yangu na mimi nimetulia tu sifanyi lolote, basi kama nilivyojaaliwa kuwa Doctor, na baadaye Mbunge, mambo ambayo katika hali ya kawaida ni magumu kwa mtu mwenye background kama yangu, haitoshindikana kwa hawa jamaa (japokuwa hawatoshi) kufanikisha ndoto zao na siku moja kuja kuwa 'Rais'. Mimi hupenda kuchukua hatua, na huwa sipendi kuwa mtazamaji tu ama mlalamikaji! Niko serious, naota ndoto ya kuwa Rais wa nchi yangu, Mungu nisaidie!"
Kwa maelezo hayo au kauli hizo Kigwangalla ni raisi Mtarajiwa, kwani anaonekana nimtu wakuishi ndani ya ndoto zake.
Mungu Ibariki Nzega itoe Rais, Mungu ibariki Tanzania na Africa nzima.
Post a Comment