Mkuu wa majeshi wa zamani nchini
Uganda ambaye sasa ni kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for
democratic Change FDC Meja Generali Mustaafu Mugisha Muntu amelaani
hatua ya sasa ya serikali ya amiri jeshi mkuu wake wa zamani ya kuandama
na kuzingira ofisi za magazeti ya The Daily Monitor pamoja na
Redpepper.
Akiongea na waandishi wa habari nchini Uganda,
Bwana Muntu alisema kuwa Rais Museveni anahofia kuwa udhibiti aliokuwa
nao kwa vyombo vya usalama na ulinzi umeanza kusambaratika na hivyo
kumtia hofu zaidi Museveni.Vituo viwili vya Redio pia vilivamiwa na kuzimwa , hii ni kwa mujibu wa gazeti la serikali la New Vision.
Wiki iliyopita magazeti ya Uganda yalidai kuwa kuna njama za kuwaua wale watakao pinga mpango wa Rais Museveni kumuandaa mwanawe kuchukua madaraka ya Uganda.
Magazeti hayo yalidai kuwa mipango hiyo ya mauaji yalitolewa na Mkuu fulani wa jeshi la Uganda.
Bwana Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, anatarajiwa kung'atuka uongozini mwaka 2016.
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kwamba Museveni anamuandaa mwanawe Muhoozi Kainerugaba,ambaye ni brigadier jeshini kushikilia uongozi wa Uganda.
Lakini serikali ya Museveni imekanusha kwamba kuna mipango kama hiyo.
Mwanawe Museveni Brig. Kainerugaba.
Wiki iliyopita gazeti la, the Daily Monitor,na jengine la , Red Pepper, lilichapisha barua ya siri ikidai ilikuwa imeandikwa na Jeneral David Sejusa, ikitaka uchunguzi ufanywe kuthibitisha madai kwamba kuna mipango ya kuwauwa wote watakao piga mipango ya Rais Museveni kumpachika mwanawe uongozini.Uvamizi huo wa polisi umeidhinishwa na mahakama ya Uganda na ulikuwa unalengo la kutafuta barua hiyo inayodaiwa kuandikwa na mkuu huyo wa Jeshi akifichua njama za mauaji.
Vituo viwili vya Redio vinavyohusiana na Daily Monitor, Dembe FM na KFM, pia vilivamiwa na kuzimwa.
Lakini wachanganuzi wa maswala ya kisiasa wanadai kuwa ikiwa barua ya Jenerali Sejusa ni ya kweli basi ni dalili kuwa kuna hali mvutano ndani ya jeshi huku ikidhaniwa kuwa wanajeshi wakongwe huenda wanapoteza uwezo kwa wanajeshi chipukizi wanaoongozwa na mwanawe Museveni Brigadia Kainerugaba.
Jenerali Sejusa ni mwanajeshi mkongwe aliyekuwa katika vita vya ukombozi uliyomuweka Rais Museveni madarakani mwaka1986.
Kwa muujibu wa taarifa za AP kamanda mmoja wa jeshi Jenerali Aronda Nyakairima amenukiliwa akisema kuwa Jenerali Sejusa kwa wakati huu anachunguzwa kutokana na barua anayodaiwa kuiandika.
Post a Comment