Home » , » Makamo wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal Avishwa Badge na Vijana UVCCM

Makamo wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal Avishwa Badge na Vijana UVCCM

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, November 27, 2013 | 2:43 PM


 Leo vijana wa UVCCM wameendelea na Zoezi lao la kuwavika Badge viongozi mbali mbali wa Nchi hii na leo ilikuwa zamu ya Mh.Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Kumbuka kuwa Vijana wamegundua kuwa wao ndio chachu ya Madiliko hivo wameanza na Kuelimishana kuhusu Ukimwi na Virusi vyake nk....

 Paul Makonda akimweleza Makamo wa Rais Kuhusu huu mpango wote wa Uhamasishaji
 Team ikisikiliza kwa Makini Makamo wa Rais alisema kuwa!
Kwanza Amewapongeza sana Vijana UVCCM kwa kubuni na kukifanyia kazi kitu hiki.
Pili, Amesema Bara la Africa ni bara ambalo liko ktk hali ngumu sana lakini pia ndilo bara ambalo limekuwa na Idadi ya waathilika wa Ukimwi wengi sana, hivo hii itasaidia sana Kupunguza Maambukizi na hatimae kukomesha kabisa.
Tatu, Nikwamba AFRICA NDILO BARA linalotizamiwa kuja kuwa Bara linalozalisha na kuiongoza Dunia hii hivo nivema kupigana na Gonjwa hili baya.

 Paul Makonda Msemaji Mkuu UVCCM lakini pia ndie Mkuu wa Msafara Akimvika Badge Makamo wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jioni ya Leo Hii.

December 1st 2013
Hii nisiku Muhimu sana katika Maisha yetu vijana wa Tanzania kwani naani hii itakuwa nisiku ya Mabadiliko yako wewe Muoga wa kupima Virusi vya Ukimwi, na Magonjwa mengine! Pia
Katika kuielekea Siku hiyo ya Jumapili ijayo Vijana tumekuwa tukivisha Viongo Badge/ Utepe mwekundu, Jana alivikwa Meya wa Jiji na Leo Tumemvisha Makamo wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Wewe Kijana wakitanzania Tunakuomba Kumtaarifu mwenzio juu ya Habari hizi kuwa Tukutane Viwanja vya Biafra kuanzia saa 7 mchana mpaka jioni saa 12.
Kuja kwako ni Faida tosha kwani utakuwa umechukua hatua ya kulisaidia Taifa lako kwa Kuelimika na kwenda kuelimisha wenzio, lakini pia utakuwa balozi wa kusema ukweli dhidi ya hayo yote tutakayo yafanya siku hiyo, kwa maana yakwamba tuelimishana, tutapima na tutafurahia pia kwa Mziki wa Asili na Nyimbo nyingine toka kwa wasanii wetu Tanzania....
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger